341 views 3 mins 0 comments

MAKONDA:SITOLIPIZA KISASI KWA MTU YOYOTE,MBOWE TUMPE PESA YA MAFUTA

In KITAIFA
October 26, 2023

Katibu mkuu wa NEC Itikadi na uenezi ccm Taifa Paul makonda amewataka mawaziri wote na wakuu wa mikoa akiwakilisha mkuu wa mkoa Albert chalamila kuwa pale patakapobainika hawajafanya kazi zao kikamilifu chama hakitasita kuchukua hatua

Akizungumza jijini Dar es salaam Leo Alhamis 26,2023 Katika viwanja vya ccm ndogo lumumba wakati akipokelewa na akikabidhiwa ofisi amesema hatokuwa teali kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi na wanaomsaidia Mhe.mwenyekiti na wanashindwa kutekeleza misimamo ya hadharani kusema uongo

“Kila kiongozi wa serikali ataubeba msalaba wake mwenyewe sijaifadhiwa kukaa miaka 3 na miezi 3 Kwa kusema uongo sijateuliwa na chama Cha mapinduzi kusema uongo na kiapo chetu kipo wazi fitina,uongo na ,uzushi, sio sehemu ya CCM”

“Haki huinua taifa na chama kimepewa dhamana ya nchi na chama kikaaminiwa Kwa kuundwa Kwa serikali ni hakika kiongozi yoyote atakae.bainika na chama kikajiridhisha chama kitachukua hatua bila ya kusubili Kwani ni wajibu wetu kukilinda kukitetea na kukipigania”. Amesema Makonda

Aidha amesema taifa hili la Tanzania halina chama Cha upizani Bali Kuna watoa taalifa wanaojikusanya Katika jina la vyama.Ukumuona Tundulisu akiongea sio chama ni mtu tu anatoa taarifa na wakati mwingine.taarifa anayoiweza kuitoa inawezekana kabisa ikawa.imetoka katika

Amesema kiongozi yeyote atakayebainika hatendi sawa na kwamba chama kikajiridhisha, hawatachelewa kuchukua hatua, akitolea mfano kama ambavyo sheria za msikiti haziruhusu mtu kuingia na viatu na kwamba akibainika, haitamngojea Imam kuchukua hatua dhidi ya mtu huyo ndivyo atakavyofanya kwenye utawala wake.
Tutachukua hatua bila kusubiri, kwa kiongozi yeyote atakayerudisha nyuma jitihada za chama kuendelea kuaminiwa na wananchi,โ€ amesema.


Mimi sina kisasi kwa Mtu yoyote, na asiwepo Mtu yoyote yule akafikiri lengo langu ni kumkandamiza, au nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikiri wamenitenda mabayaโ€


Makonda akitumia nafasi hiyo amewashukuru waandishi wa vyombo vya habari nchini kwa kuendelea kushirikiana na CCM na kwamba waandishi wa habari wamekuwa kiunganishi kikubwa kati ya Chama na wananchi , hivyo Chama hicho kitaendelea kushirikiana na vyombo vya habari.

Aidha Makonda amemtakia majukum mema aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Sophia Mjema na kwamba anaamini watashirikiana katika kuyasemea makundi mbalimbali

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza amesema ili CCM iendelee kuaminiwa na Watanzania, ni lazima watekeleze ilani ya chama hicho kwa kujibu kero wanazopitia wananchi.

โ€œNimesikiliza hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, aliyoyasema ni ukweli kwani ana nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya chama, na ili kiweze kuendelea kuaminiwa, ni lazima ahadi zilizotolewa kupitia ilani, zitekelezwe,โ€amesemansrq c,

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram