153 views 2 mins 0 comments

GADDAFI:AWAPA KICHENIPARTY VIONGOZI WASIOTAKA VIONGOZI WA NGAZI YA CHINI KUFANYA MIAZARA

In KITAIFA
October 26, 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Komredi Abbas Mtemvu amewataka viongozi wa serikali waliopata nyadhifa kuanzia ngazi ya Serikali za Mitaa ,Wilaya hadi Mkoa kushirikiana na Madiwani na Wabunge wa Viti maalumu wanapotaka kufanya ziara katika kata kujua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.


Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam Katika Shughuli ya Kukabidhiwa Vitendea kazi kwa viongozi wa UWT kata 102 wilaya tano za mkoa huo Kinondoni,Ilala,Ubungo,Kigamboni,Temeke vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu MAriam Kisangi ambapo amesema Madiwani na Wabunge wa Viti maalumu wanamchango mkubwa katika.utatuzi wa changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi

“Nawasisitiza sana Mshikamane na Mpendane acheni kuwabania Wabunge na Madiwani wa Viti maalumu wanapowaomba kuja kutembelea kata zenu kuangalia Ahadi za Ilani ya CCM ilivyotekeleza miradi na kusaidia pale wanapoona Kuna changamoto wao hawaji kufanya kampeni kuomba kura Kwa wananchi ondoeni vinyongo rohoni Ili tushinde uchaguzi 2025 inahitajika nguvu Moja”amesisitiza Komredi Mtemvu

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Taifa CCM NEC Juma Gadafi amesema kuwa viongozi wa ngazi ya juu CCM hawakubaliani kuona Wabunge na Madiwani wa Kuteuliwa kuzuiwa kufanya ziara katika kata kwa kuwekewa vipingamizi na wakimbaini kiongozi yeyote anaehusika Katika hilo atashughulikiwa kwani hafai kabisa anataka kukwamisha maendeleo.

“CCM inakwenda kushirikiana na kila mtu bila kuangalia itikadi yake Ili kuleta maendeleo kwa wananchi lakini inashangaza kabisa kila kukicha tunaletewa malalamiko ya Wabunge na Madiwani wa Kuteuliwa kuzuiwa kufanya ziara na kusaidia kutatua kero za wananchi hebu jifunzeni Leo hii Mbunge huyu alichokifanya kwa kutoa fedha zake kununua meza,Viti majiko ya gesi yatakayokwenda kuwasaidia wenyewe kupendezesha ofisini kwenu mnakohudumia wananchi”Amesema Gadafi

Aidha ameonya vikali viongozi hao badala ya kufanya kazi za kuhudumia wananchi wanaotumia Muda mwingi kudhohofisha jitihada za Wabunge na Madiwani wa Viti maalumu waliowapendekeza wenyewe

Nae Mbunge wa Viti maarum MAriam Kisangi amesema Ilani ya chama Cha mapinduzi CCM imewekwa vizuri na tumeona Shughuli ambazo RAIS Samia Suluhu Hassan akizifanya Kwa juhudi Kwa kutengeneza miladi mbalimbali kama Shule, Barabara ambazo zimetengenezwa Kwa weledi na ameweza kukamilisha Kwa WAKATI na wakandarasi wengine Bado wapo kwenye kazi

Pia Amesisitiza kuwa ifikapo 2025 zile changamoto za mkoa wa Dar es salaam zitakuwa zimeshakamilika Kwa kiasi kikubwa

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram