330 views 58 secs 0 comments

SIMBA WATOLEWA KATIKA MICHUANO YA AFL2023

In MICHEZO
October 24, 2023

AFL2023: Licha ya safari ya Klabu ya Simba kukatishwa na Goli la Ugenini lililoibeba Klabu ya Al Ahly, Wekundu hao wa Msimbazi wamejihakikishia malipo ya Dola za Marekani 1,000,000 zilizotangazwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linalosimamia Ligi ya African Football(AFL)

Michuano hiyo iliyoanzia hatu ya Robo Fainali, ilianza kwa kuvijumuisha Vilabu vya Enyimba FC (Nigeria), Wydad AC (Morocco), Mamelodi Sundowns FC (South Africa), TP Mazembe (DR Congo), Espรฉrance Sportive de Tunis (Tunisia), Atlรฉtico Petrรณleos de Luanda (Angola), Al Ahly SC (Misri) na Simba SC (Tanzania)

Mshindi wa Kombe la Ligi hii ataondoka na Dola za Marekani 4,000,000 baada ya kukamilisha Michezo 6

Timu gani unaitabiria nafasi ya kuondoka na zaidi ya Tsh. Bilioni 10 zilizotengwa?

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram