

DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa jumuiya ya waandishi wa Habari JUMIKITA Shabani omari matwebe Amesema jambo lolote ambalo linakuwa na tija na linahusika na wananchi inapaswa waandishi wa habari kuliunga mkono Kwa kulichukua na kulifikisha Kwa jamii
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumanne 24,2023 Mwenyekiti wa jumuiya ya waandishi wa habari JUMIKITA Shabani omari matwebe Amesema Sisi kama WANAHABARI inapaswa kuchukua maoni au jumbe mbalimbali kutoka serikalini kwenda Kwa wananchi na tunaishukuru serikali Kwa sababu wananchi walitoa maoni kupitia mkataba na ule upotoshaji uliokuwepo tokea mwanzo kwenye namna ya mkataba ule ulivyokuwa unasomwa
“Sisi kama WANAHABARI kulitumia weredi wetu wa kufikisha jumbe ambao tunaamini haukubomoa Bali umejenga na mafanikio makubwa ya KUSAINI mkataba wa Dp world na mkataba huo umesainiwa Kwa kuzingatia maoni ya wananchi Asilimia 99 ya wananchi Kwa ajili ya maslahi ya nchi”. Amesema Matwebe

Aidha Matwebe Ameipongeza serikali Kwa KUSAINI mkataba huo wa miaka 30 Kutokana na Wafanyabiashara walivyokuwa wanalalamika na kuwa na mnyororo wa ufisadi mkubwa ambao ulikuwa unafanywa na baadhi ya mataikudi ambao walikuwa wanaitumia bandari kama pango la wizi na wamachinga hao wanafurahi kuona dp world wanakuja na kuwekeza na bandari haitakuwa tena Katika pango la ulanguzi ambao watakuwa watu rasmi wa kusimamia MAPATO na kile ambacho kitakuja Kwa wananchi kwahiyo wafanyabiashara furaha Yao mkataba kusainiwa na watu wazuri Katika bandari na kuwa lile pango la ulanguzi rasmi limeenda kufungwa na serikali watapata wanachokusudia
Nae Makamu wa wamachinga Tanzania na Kariakoo Steveni Rusinde Amesema Tulipokea wazo Kwa wenzetu la mama Nivushe maana mama ametuvusha kwenye mambo mengi Kama wajawasiriamali Kwa kutupa wizara maarum wizara ameiuunda na mwezi haujaisha.na kutupeleka Katika wizara ya makundi maarum ya Jinsia ya wanawake

Amesema mama Nivushe maana yake kubwa lipo kwao na Mhe RAIS Kwa kuandaa BAJETI mbalimbali kwenye kundi letu na kutoa fedha Kwa kila mkoa milion 10 Kwa kuhakikisha wamachinga wanapata ofisi na sisi kama wamachinga Kwa kushirikiana na wezentu tunaunga mkono kampeni ya mama Nivushe
“Tumeona shule nyingi zikijengwa , masoko na kutoa baadhi ya pesa Katika miradi mbalimbali na sisi kama wamachinga tutazidi kutoa Elimu Kwa wamachinga wenzetu kuhusiana na MAMA NIVUSHE 2023”. Amesema Rusinde
MADINA MOHAMMED