

Muimbaji wa Gospel Joyce Mwaikofu Ameiomba serikali kutoa Elimu Kwa wasanii na waimbaji ambao hawajui BASATA na Cosota Ili kuweza kutoa Elimu Kwa waimbaji hao
Amesema fursa nyingi huwa zinakuja za nje na ndani Kupitia serikali na serikali haiwezi kutoa msaada Kwa mtu mmoja wanaitaji waunde vikundi au vyama vya waimbaji Ili pindi fursa hizo zinapokuja ziwafikie Kwa wote na amesema waimbaji wa injili wapo nyuma sana na hawaelewi
Akizungumza wakati Akiitambulisha Nyimbo yake ya Nitaifuta Machozi Hapo Jana Katika kumbi za center point Mwaikofu amesema Mziki ni TIba kwani Kuna watu wanapitia matatizo ya kisononi na magonjwa mbalimbali yanashuka Kwa Kupitia mziki Unaweza kujitibu
Aidha Mwaikofu amesema Kwa Sasa Kuna changamoto Katika YouTube amesema kunaitaji uwekezaji wa nguvu na Ili kuweza kujulikana na kupata promo unaitaji umpate Mtu ambae anaeijua IT Ili kuweza kuweka mitandao Yao vizuri na changamoto ya watu wengi hawana kipato
Hata hivyo Mwaikofu Ameishukuru serikali Kupitia waziri na Naibu waziri wa Utamaduni sanaa na michezo kuona changamoto zao wanazozipitia Katika uimbaji wao
Madina Mohammed