230 views 2 mins 0 comments

POLISI “WADEPO 1993″WATOA MSAADA WA THAMANI SH MILIONI 2.5

In KITAIFA
October 21, 2023

Baadhi ya Askari Polisi waliotimiza miaka 30 katika utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi ‘Wadepo 1993’ leo Oktoba 21, 2023 wametembelea Hospitali ya Polisi Kilwa road na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 2.5.


Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa umoja wa Askari hao, ACP. Ally Wendo amesema fedha hizo zimetokana na michango yao ambayo wamechanga na kununua vitu
mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaopata huduma Hospitalini hapo.


“Tumeamua kufanya hivi kwa nia ya kumshukuru mungu kwa afya na uzima katika kipindi chote cha miaka 30 ya utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi kwa maana kuna baadhi ya wenzetu ambao
tulitamani kuwa nao likini hatuponao kwa sababu mbalimbali”. Amesema ACP Wendo

Msaada uliotolewa ni pamoja na
mashuka, Madawa mbalimbali, mito ya kulalia, sabuni za kufulia na katoni za maji ya kunywa.


Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, ACP. Dkt. Hussen Yahaya amewapongeza askari hao kwa kuwa na umoja ambao wameamua kutoa msaada katika Polisi ya Kilwa road

“kwa kufanya hivi mtakuwa mmejisaidia nyinyi wenyewe, familia zetu pamoja na
wananchi ambao wanapata huduma katika hospitali hiyo yenye hadhi ya rufaa ya Mkoa”.Amesema ACP Yahaya


Katika hatua nyingine Dkt. Yahaya amesema hospitali hiyo ipo katika ujenzi wa jengo la hospitali la ghorofa tatu ambapo ametoa wito kwa vikundi kama hivyo, taasisi na asasi za kiraia katika
kusaidia katika ujenzi na vifaa Hopitali hiyo ya Polisi ili iweza kutoa huduma zaidi za matibabu

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram