Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Ndugu Kiula Kingu amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la “Dawasa yetu” lililo fikia asilimi 90 hatua za mwisho za utekelezaji.
Amezungumza hayo Wakati wa ziara yake Aliyoifanya Jijini Dar es salaam amesema wamefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo huku akisema uwepo wake utafanya watanzania wanufaike na kuondoka kwa kero haraka kwa kua wataweza kuhudumia vizuri wateja wake
“hili ni jengo la DAWASA linaitwa DAWASA YETU jengo hili lina floor 13 na zimegawanywa katika idara tofauti sisi tuna idara 14 hivyo kila idara na floor moja watakuepo watumishi wote kwasasa limekamilika kwa asilimia 90 zimebaki kama asilimia 10 mradi umechukua kama Billion 46 ukikamilika utafanya wafanyakazi wawe na uwezo wa kufikiri na kutatua kero za wateja wetu kwa ufanisi na haraka’’.Amesema Kingu
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi DAWASA Generali mstaafu Davis Mwamunyange amesema DAWASA inahitaji kua na mifumo ya kisasa zaidi huku akiongeza wanajitahidi kuendana na kasi za teknolojia kuendana na mabadiliko ili wawape huduma bora wateja wao
Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi kampuni ya Civil Engineering Construction Corporation (CCECC)