239 views 12 secs 0 comments

SERIKALI KUWAPA FURSA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI

In KITAIFA
October 14, 2023

Dar Es Salaam

Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma muhimu katika maeneo ya vijijini ili kuwapa fursa wananchi hasa Wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi kufikia maendeleo endelevu na jumuishi kwa wote.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani Dar Es Salaam, Oktoba 12, 2023 kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yatakayofanyika Oktoba 15, 2023 mkoani Arusha.

Waziri Dkt Gwajima amesema miongoni mwa jitihada hizo ni kuendelea kukuza kilimo kwa kuhakikisha uwepo wa pembejeo na zana bora za kilimo na upatikanaji wa maji ili kumpunguzia mwanamke muda wa kufuata maji ili autumie katika uzalishaji mali.

Amefafanua kuwa juhudi nyingine ni pamoja na kuondoa tozo, kodi na kufungua milango ya biashara nchi za nje ambapo tozo 100 zimeondewa ili kupunguza gharama za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

“Serikali imewezesha wakulima ambao wengi wao ni wanawake wanaoishi vijijin

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram