Hayo Yamesemwa leo na Mkurugenzi na Muandaaji wa Maonesho hayo Bw. Deogratius John Kilawe , alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa Maonesho hayo yana lengo la Kuwakutanisha kwa Pamoja Wadau wa Sekta ya Ujenzi na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua Sekta hiyo pamoja na kukuza Mahusiano na kujipatia Wateja wa Bidhaa zao.
Pia amesema Maonesho haya yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia Tarehe 11- 13 Oktoba 2023 na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.
Aidha Bw. Kilawe amesema kuwa, huu ni msimu wa 7 wa Maonesho ya Dar Constuctions Expo na yanajumuisha zaidi ya Makampuni 120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta Tija na Mapinduzi katika sekta ya ujenzi na kukuza na kuendeleza Uchumi wa nchi pamoja na Kuchangia Pato la Taifa.
Akiendelea kufafanua jambo Bw. Kilawe ametoa Wito kwa Watanzania na watu wa Mataifa mbalimbali kuhudhulia Maonesho hayo ili kuja kujifunza na kujionea Teknolojia mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Ujenzi, zitakazooneshwa na Makampuni hayo ili kuwasaidia Watanzania kupanua wigo mpana wa Uzalishaji wa bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu zitazoleta Ushindani katika Soko la Kimataifa.
“Natoa Wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika Maonesho haya ili kupata fursa zitakazopatikana katika Maonesho, na pia nashauri Wadau wa Sekta mbalimbali za Ujenzi wahakikishe wanashiriki katika Maonesho ili kuongeza uzoefu Pamoja na kujifunza Teknolojia mpya itayopatikana katika Maonesho hayo” Alisema.
Madina Mohammed