218 views 2 mins 0 comments

TUNZO ZA MAGIC VIBE AWARD KUPAMBA MOTO

In BURUDANI
October 09, 2023

Muigizaji na mtangazaji wa clouds media Burton Mwambe maarufu kama mwijaku azungumzia Sakata LA kufungwa kwa shule mjini Paris kuwa na wingi wa kunguni.

Mwijaku amesema kuwa alipata bahati ya Kufika katika jiji hilo na kuona muingiliano mkubwa wa watu wanaoenda kutalii katika jiji hilo huenda ndio wanaosababisha kunguni mjini Paris.

Mwijaku amesema hayo oktoba 9 jijini dar es salaam wakati akitambulisha msimu wa pili wa tuzo za magic vibe Award inayotarajia kufanyika November 19 mwaka huu

Aidha mwijaku amesema wanaenda kuleta mageuzi Katika mziki na amewataka wasanii kutoleta kasumba Katika tunzo hizo

“Kama unajiamini kwenye kazi yako waache mashabiki wakupigie kula na kujua kama mashabiki wako wanakupenda na hicho ndicho kitakuwa kipimo chako sio Instagram kuwa na like nyingi au tweet na kipimo Cha kupendwa ni namna Gani Jinsi watakavyokupigia kula”amesema mwijaku

Aidha amewafunda wasanii ambao wanaotoa nyimbo zao ambazo zinazoweza kumgusa mtu hata kupata muamko wa kumpigia kula na sio kila siku msanii anaimba

“Mimi nimekaa Paris nimezunguka kwenye maklabu Zaidi ya tano na kukuta nyimbo ya alikiba zikipigwa na kuona muamko wa watu”ameongeza mwijaku

Nae Sayf Mzilay amesema Tanzania ni Hub ya Entertainment Eastern Friends kwa sababu ushindani ni mkubwa na Lengo ni Kuimarisha,kujenga thamani kwa msanii wetu na heshima

“Idadi ya makundi mwaka huu tuna karibu vipengele 27,lakini kwa mwaka jana tulikuwa na vipengele 20 tu na tumeongeza makundi saba (07) baadhi yao ni DJ, wazalishaji, wajasiriamali, ACT ACT reasons Sababu ni Mafanikio na Ustawi ni pamoja na ubunifu, Hit nyimbo na athari na ushawishi”amesema mzilay

Hata hivyo mzilay ametoa Jinsi ya Upigaji kura wa Umma kupitia tovuti yetu (www.magicvibeawards2023.com)

MADINA MOHAMMED

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram