Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa jitihada za dhati katika kuleta maendeleo ya uhifadhi nchini ikiwa ni pamoja na Usimamizi mzuri wa Wanyamapori
Mhe. Kairuki ametoa pongezi hizo Oktoba 7, 2023 alipotembelea bustani ya Wanyamapori hai katika maonesho ya Saba ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo – SITE yanayofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam
“niwashukuru wote lakini zaidi niwashukuru TAWA kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaifanya kwa ajili ya maendeleo ya uhifadhi pamoja na kuendelea kusimamia hifadhi zetu mbalimbali na kuhakikisha pia kunakuwa na Utalii ambap ni endelevu unaozingatia masuala mazima ya uhifadhi” alisema Mhe. Kairuki
Aidha Waziri Kairuki amesema Wizara yake kupitia TAWA imepeleka bustani ya Wanyamapori hai katika maonesho hayo ili kuendelea kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na kuvitumia na kuona rasilimali tulizonazo kama Taifa.
Maonesho haya yanafikia tamati leo Oktoba 8, 2023.