KATIKA kuimarisha Diplomasia ya Uchumi nchini,Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu nchini india kuanzia October 8 hadi 11 Mwaka huu.
Akizungumza na waaandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Leo tarehe 05,2023 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa January Makamba amesema kuwa Madhumuni ya ziara hiyo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassani ni kukuza ushirikiano wa kidiplomasia ya kiuchumi baina ya Tanzania na india katika sekta za kimkakati za Ulinzi, Maji, kilimo, Afya, Biashara na uwekezaji.
” Moja ya Mashirikiano yetu na nchi ya india nikukuza eneo la kimkakati hasa viwanda vya kutengeneza simu za Smattphone hapa nchini, pamoja na taasisi za kiafya za upandikishaji figo pamoja kiwanda cha chanjo za Binadamu”.Alisema Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba.
Waziri Makamba alisema sambamba mashirikiano hayo katika sekta ya Afya pia ziara hiyo ina lenga kukuza Masoko ya Mazao ya kilimo ikiwemo Bidhaa za Mbaazi nchini humo.
Alisema pia ziara hiyo inalenga uwekezajiwa Viwanda vya karakana vyombo vya Usafiri Majini sambamba na Mradi wa Maji wa ziwa Victoria.
“Mikataba 15 inatarajiwa kusainiwa kati ya Tanzania na india ya ushirikiano katika kutekeleza Diplomasia yauchumi kutafuta masoko na kuimarisha uwekezaji “Aliongeza Waziri January Makamba.
Madina Mohammed