222 views 2 mins 0 comments

MAVUNDE:KUSAIDIA WA TANZANIA KUPATA MKOPO NA KUINGIA KATIKA SEKTA YA MADINI

In KITAIFA
October 05, 2023

Mkutano mahususi kati ya Taasisi za fedha ambao unahusisha wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa na watoa huduma Kwa kujadiliana kwa changamoto kubwa ya Taasisi za fedha kuto wakopesha sekta ya madini

Changamoto hiyo inawafanya watanzania wengi kuwa waangaliaji wa Fursa kubwa ya madini iliyopo Nchini Tanzania na sio washiriki wa sekta ya madini

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo 05,2023 Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema kama wizara wameona kuwawezesha watanzania nao washiriki na wanufaike na madini Yao

“Kupitia mkutano huu tutatengeneza ramani nzuri wa ushirikishwaji wa sekta ya fedha na kwenye kuchochea sekta ya madini na lengo letu ni kuwaona watanzania wengi Zaidi wanakopeaheka bila kiwaathiri sheria za fedha”. amesema Mavunde

Aidha Mavunde amesema Tumewaita mabank yote ya hapa Nchini na tutazungumza Kwa pamoja watuambie wasiwasi wao ni nini na nini kifamyike upande wa serikali au upande wa wachimbaji Ili Kwa pamoja tuweze kutoka na Kauli Moja ya kuwainuwa watanzania Kwa kushiriki Katika sekta ya madini


Aidha Waziri wa Madini Anthony Mavunde ametoa onyo na kusema hatamuonea aibu mtu yeyote atakayejihusisha na utoroshwaji wa Madini na ikibidi atafuta leseni yake.

Akifungua mkutano wa majadiliano kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa sekta ya madini nchini unaofanyika mkoani Dar Mavunde amesema, atafuta leseni na kumuweka katika orodha isiyofaa mchimbaji yeyote atakayebainika kutorosha madini.

Nae Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini nchini John Bina amesema utafiti katika sekta ya madini nchini ndio utasaidia kuonesha njia ya ukuaji wa sekta ya madini.

Akizungumzia sekta ya Wachimbaji madini nchini Bina amesema, mwelekeo wa 2030 katika madini unatoa maelekezo ya kufanyika kwa utafiti katika sekta hiyo hapa nchini.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram