260 views 37 secs 0 comments

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI MILIONI 500 TAIFA STARS

In MICHEZO
October 04, 2023


Leo Oktoba 4, 2023, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa  Kassim Majaliwa amekabidhi hundi ya Tshs Milioni 500 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) katika uwanja wa Taifa Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salaam.

Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu  Hassan katika halfa ya kukabidhi hundi hiyo Mhe. Majaliwa ametoa pongezi kwa viongozi na wachezaji wa Taifa Stars kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya mashindano ya AFCON ambayo yanatarajiwa kufanyika mwakani 2024, nchini Ivory coast.

“Leo  tutashuhudia kutunukiwa wachezaji wetu shilingi million 500 baada ya kuwa wamefuzu AFCON 2023. Mhe. Rais ametimiza ahadi yake, lengo kuu la fedha hizi ni kuleta chachu na hamasa kwa wachezaji kuendelea kutuheshimisha kama Taifa na kuhakikisha sekta ya michezo inakuwa na kulitangaza vyema Taifa letu ili kuchochea fursa za uwekezaji Nchini”

Katika hatua nyingine Mhe.Majaliwa amekagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa na kuridhishwa kazi inayofanyika ikiwa ni maboresho kuelekea mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano ya African Super League mchezo utakaohusisha klabu ya Simba kutoka Tanzania ya Al Ahly kutoka nchini Misri.

Taifa Stars imefanikiwa kufuzu AFCON baada ya kutoka sare ya 0-0 na timu ya Taifa ya Algeria.

/ Published posts: 1488

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram