386 views 40 secs 0 comments

COMRADE JOKATE MWEGELO APOKELEWA KWA SHANGWE DAR

In KITAIFA
October 04, 2023


> _Atoa shukrani kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini na kumteua._

> _Ahaidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa kutosha._

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (UWT) Ndugu. Jokate Mwegelo amepokelewa rasmi alipowasili katika Ofisi za CCM Makoa Makuu Lumumba Jijini Dar es salaam.

Cde. Jokate amefika katika Ofisi hizo kuchukua Barua yake ya Uteuzi wa Nafasi hiyo ya Ukatibu Mkuu wa UWT – Taifa.

Akizungumza mara baada ya kupokea Barua hiyo, Cde. Jokate ametanguliza shukrani kwa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Daktari. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo.

Aidha, Cde. Jokate ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wanawake wote Nchini haswa katika kupeana fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Aidha, Cde. Jokate ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia yenye malengo thabiti ya kuendelea kuleta Maendeleo katika kila sekta ikiwemo Afya, Elimu, Maji na Miundombinu ya barabara.

Mapokezi rasmi na Makabidhiano ya Ofisi yatafanyika makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma, Tarehe 12 Oktoba, 2023.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram