190 views 3 mins 0 comments

NDEGE AINA YA BOING KUWASILI KESHO KWA BASHASHA

In KITAIFA
October 02, 2023

Tanzania inatarajia kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boing B 737-9 Max ambayo itapokelewa katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julias Nyerere Oktoba 3,2023.

Mapokezi hayo yataenda sambamba na uzinduzi wa ndege mbili za mafunzo aina ya Cessna 1725 ambazo zitakabidhiwa kwa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT)

Hayo yamesemwa Leo na waziri wa uchukuzi prof makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bandari jijini Dar es salaam amesema Kwa mwaka 2016 serikali ilichukua hatua za kuifufua kampuni ya ndege Tanzania ATCL Kwa kuanza kuinunulia ndege na kufanya Mabadiliko ya menejimenti na bodi ya wakurugenzi


“Septemba, 2023 ATCL imeshapokea ndege 12 mpya ambazo zimenunuliwa
na Serikali. Ndege hizo ni: ndege mbili kubwa aina ya B787-8 Dreamliner
ambazo zinauwezo wa kubeba abiria 262 kila moja; ndege nne za masafa
ya kati aina ya Airbus A220-300 ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 132
kila moja; ndege tano za masafa mafupi aina ya D8 Q400 ambazo zina
uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na ndege kubwa ya mizigo aina ya
B767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54″. Amesema Mbarawa

Aidha Mbarawa Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Dkt, Samia Suluhu
Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea
kuhahakikisha kuwa Kampuni ya Ndege Tanzania inatoa huduma zenye
kuhimili ushindani kwa kuanzisha safari za moja kwa moja kwenda kwenye
masoko ya kikanda na kimataifa.

“Mwezi Julai, 2021 Serikali iliingia mikataba
na Kampuni ya Boeing ya Marekani ya ununuzi wa ndege nne mpya zenye
teknolojia ya kisasa. Ndege hizo ni ndege mbili za abiria za masafa ya kati
aina ya B737-9MAX zenye uwezo wa kubeba abiria 181 kila moja, ndege
moja ya abiria ya masafa marefu aina ya B787-8 Dreamliner yenye uwezo
wa kubeba abiria 262 na ndege moja kubwa ya mizigo aina ya Boeing B767-
300F yenye uwezo wa kubeba tani 54″. Ameongeza Mbarawa

Pia Ameongeza Kwa kusema kuwa Ndege ya mizigo aina ya B767-300F
tayari ilishawasili na inaendelea kutoa huduma zake na ndege moja ya
masafa ya kati aina ya B737-9Max uundaji wake umekamilika na inatarajia
kuwasili nchini tarehe 03 Oktoba, 2023. Ndege mbili zinaendelea kuundwa
ambapo zinatarajia kuwasili nchini mwezi Disemba, 2023 na mwezi Machi,
2024.

Ndege ya abiria ya masafa ya kati aina ya B737-9MAX ambayo uundaji wake
umekamilika inatarajia kuwasili nchini tarehe 03 Oktoba, 2023. Ndege hiyo
inauwezo wa kubeba abiria 181 katika madaraja mawili ambapo daraja la
kawaida โ€œeconomy classโ€ ni abiria 165 na daraja la biashara (business class)
abiria 16, pia uwezo wa kubeba mzigo wa tani 6 na kuruka wastani wa
masaa 8 bila kutua.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram