479 views 43 secs 0 comments

RC CHALAMILA ATAKA WANANCHI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

In KITAIFA
October 01, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Octoba 1, 2023 amefika eneo la ajali ya moto Kariakoo Jijini Dar es Salaam ambapo janga hilo la moto limetokea majira ya asubuhi na kusababisha kuteketea jengo moja pamoja na baadhi ya bidhaa zilizokuwemo katika Jengo hilo.

RC Chalamila akitoa taarifa ya Serikali kufuatia janga hilo amesema hadi saa 4:15 asubuhi taarifa aliyo nayo hakuna mtu aliyepoteza maisha au majeruhi kufuatia janga hilo, ametoa pongezi kwa vyombo vya ulinzi na Usalama hususani jeshi la zima moto kwa kuzibiti moto huo usisambae lakini pia jeshi la polisi kuhakikisha hakuna wizi au upotevu wa mali za wafanyabishara.

Aidha RC Chalamila amewataka wananchi kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya majanga ya moto wakati wote pia amekemea kitendo cha kiziba vipenyo au njia kati ya jengo moja na jingine ambayo husababisha majanga ya moto yanapotokea magari ya zima moto hushindwa kupita hivyo waliojenga kuzuia vinjia hivyo kwa mujibu wa ramani ya mipango miji kuvunja mara moja

Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amewataka wafanyabishara wa Kariakoo na Wananchi kwa ujumla kuwa watulivu, ambapo amelipongeza Jeshi la zima moto, Polisi na wadau wengine kama DAWASA kwa kushiriki kikamilifu kuzuia kusambaa kwa moto huo ambao ungeweza kuleta madhara makubwa zaidi.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram