293 views 42 secs 0 comments

MSALABAS YAWEKEZA ZAIDI YA BILIONI TANO ZA KITANZANIA GEITA

In Uncategorized
September 28, 2023


ZAIDI ya Shilingi za kitanzani Bilioni 5 zimewekezwa katika Maabara ya MSALABS inayopima sampuli za Madini kwa kiwango cha kimataifa mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa Septemba 27, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maabara ya MSALABS Mugisha Lwekoramu wakati wa ufunguzi wa Maabara hiyo iliyoanzishwa mwaka 2020 ikiwa ni kampuni tanzu ya MSALABS yenye makao makuu yake nchini Canada.

Akizungumzia kuhusu teknolojia inayotumika katika Maabara hiyo Lweramu amesema Maabara hii inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa mionzi yaani (PhotoAssay) ambayo ni rafiki kwa utunzaji mazingira kwasababu haitumii kemikali au moto katika upimaji sampuli.

Akielezea kuhusu ufanisi wa teknolojia hiyo amesema hii ni sehemu ya mapinduzi ya teknolojia kwasababu inamwezesha mdau kupata majibu ya sampuli ndani ya masaa mawili ni tofauti ukilinganisha na teknolojia ya zamani ya kutumia moto na kemikali.

Kwa upande Waziri wa Madini Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini , akiwataka kuendelea kufungua matawi mengine nchini.

Mavunde amehaidi kuwa Serikali Awamu ya Sita itaendelea kuwatengenezea mazigira rafiki ya uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa jinsi itakavyohitajika katika mnyororo mzima wa sekta madini.

Aidha, aliwapongeza kwa kuweza kuajiri watanzania kwa asilimia 99.8 akiamini kuwa wafanyakazi hao wataendelea kujifunza utumiaji wa teknolojia hiyo na kutoa ujuzi huo kwa watanzania wengine.

/ Published posts: 1487

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram