275 views 2 mins 0 comments

Hisia za viongozi wa Afrika Mashariki baada ya kukubaliwa kuandaa AFCON 2027

In KITAIFA, MICHEZO
September 28, 2023

Viongozi wa Afrika Mashariki wamepongeza kutunikiwa hadhi ya kuandaa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), 2027, baada ya ombi la pamoja la Uganda, Tanzania na Kenya kukubaliwa.

Itakuwa mara ya kwanza kwa shindano hili kuu la kandanda barani Afrika kuchezwa katika mataifa matatu kwa wakati mmoja, baada ya lile lililofanyika Ghana na Nigeria kwa wakati mmoja mwaka 2000 na Equatorial Guinea na Gabon mwaka 2012.

‘’Tunashukuru kupata fursa ya kuandaa AFCON 2027 kwa ushirikiano na Kenya na Uganda’’, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye X (zamani ikitwa Twitter)

‘’Ninawashukuru wote walioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu.’’

Sasa naiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kufanya maandalizi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa viwanja viwili vipya Dodoma na Arusha kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa’’, aliongeza.

Naye Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kupokea shindano hilo kutaathiri vyema uchumi wa mataifa hayo.

‘’Nilipata habari njema kwamba ombi letu la pamoja na Kenya na Tanzania la kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 limefanikiwa. Nawashukuru waandaaji kwa kuweka hoja nzuri kwa mataifa ya Afrika Mashariki. Hii itakuza nchi zetu na kuleta athari njema kwa uchumi wa mataifa yetu, hasa sekta ya utalii.’’ Bw Museveni aliandika kwenye X.

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua pia alipeleka hisia zake kuhusu suala hilo kwenye ukuraza wa X, kuonyesha kufurahishwa kwake na hatua ya kuletwa kwa AFCON Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza tangu Ethiopia iandae shindano hilo mwaka 1976.

‘’ Inafurahisha kupokea taarifa kwamba ombi la pamoja la Kenya, Uganda na Tanzania la kuandaa AFCON 2027 limekubaliwa…na Shirikisho la Soka la Afrika.’’ Alisema Gachagua

/ Published posts: 1488

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram