314 views 42 secs 0 comments

WANAJESHI WAOKOLEWA BAADA YA KAMBI YA JESHI LA MALI KUSHAMBULIWA

In KIMATAIFA
September 27, 2023

Wanajeshi wamehamishwa kutoka kambi ya jeshi kaskazini mwa Mali kufuatia shambulio la watu wenye silaha, jeshi la taifa hilo limesema.

Wanajeshi wa Mali waliwakabili washambuliaji huko Acharane, eneo karibu na mji wa kale wa Timbuktu, taarifa ilisema.

Bado haijabainika iwapo watu hao wenye silaha walikuwa wanamgambo wa Kiislamu au waasi wa Tuareg.

Makundi yote mawili yameongeza mashambulizi yao katika wiki za hivi karibuni – wakati ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaondoka nchini humo baada ya kuamriwa kuondoka na watawala wa kijeshi wa Mali.

/ Published posts: 1898

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram