176 views 5 mins 0 comments

KANYASU AMEIOMBA TUME YA MADINI KUJA NA TEKNOLOJIA YA KUKAMATA SHABA DHAHABU NA FEDHA

In BIASHARA, KITAIFA
September 27, 2023


Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh. Constantine John Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya Madini na pia kupata nafasi ya kuwa Mgeni mahususi katika kutembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonesho hayo

Amesema Maonesho haya yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi na hii inaleta hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi umeongezeka, pia kuongezewa Kwa makampuni ya Madini hasa wanaonyesha Teknolojia ya Madini.

Kanyasu amesema Kwa mara ya kwanza Maonesho hayo yameleta Watanzania wanaochimba madini ya vito ( Tanzanite) kutoka kule Naisinyai Wilaya ya Simanjiro mkoani manyara na Mikoa mingine na hata nje ya nchi kuja kutangaza Biashara zao Tanzania, hivyo amewapongeza waandaaji Kwa jambo hilo kubwa na muhimu.

” Lakini pia kwa mara ya kwanza tumeona kupitia Maonesho haya namna ambavyo yameweza kuleta watu mbali mbalimbali ikiwemo wajasiriamali wafanya biashara kutoka Mikoa mbalimbali na hata nje ya nchi kuja Tanzania kutangaza biashara zao hivyo nachukua fursa hii kuwapongeza waandaji wote na ni matumaini yangu mwakani tutapata washiriki wengi zaidi amesema Mbunge Kanyasu.

Aidha amesema jambo pekee ambalo wananchi wanatakiwa kujua ni kwamba bado walengwa haswa ( wachimbaji) wenyewe bado hawajafikiwa kwa kiasi cha kutosha hivyo ametoa rahi kwa mamlaka husika kuweza kuwafikia.

” iko haja ya Makampuni ya kwenda chini kwa lengo la kuwafikia wachimbaji hiyo ndiyo maana harisi ya, Maonesho haya na sio makampuni makubwa kama GGM, Bakrifu, na Sota Mining, haya maonesho yanalenga wachimbaji wadogo kwahiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini kwa lengo la kuwapeleka Teknolojia, mitaji, lakini kuwawekea bima” amesema Kanyasu.

” Amesema kwakuangalia tu hapa walikuja ni mabosi ila wachimbaji wenyewe yaani wanaingia maduarani hawajafika hapa na hawajapata nafasi ya kuja kuona Maonesho haya, na ndio pindi zinapotokea ajali kwenye maduara wao ndowanaokufa Kwa kuangukiwa na miamba” ameongeza Mbunge Kanyasu

Aidha amesema kadiri inavyoonekana Geita ilivyo sasa sivyo ilivyokua zamani, kuanzia Kasamwa mpaka Geita mjini palikua na msitu Mkubwa sana, lakini miti yote imekwisha kwasababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) ambapo amesema iko haja ya kutafuta Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote inayobaki tutaharibu hali ya hewa.

“Kuna uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwahiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti, kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini kwaajili ya kufidia ile Misitu ambayo imeharibika, mimi nafikiri kwakufanya hivyo tutaendelea kuwa salama zaidi kwa hali hiyo” amefafanua Kanyasu.

Ameiomba Wizara ya madini kuhakikisha kwenye Maonesho kama hayo mwakani, tuwe na Banda linaloonyesha bidhaa mbalimbali zilizokamili za mawe aina mbalimbali, maana tulipofanya Maonesho ya Madini Dar es Salaam tulikua na watengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama mikufu, Mikanda, shanga, heleni, shanga, vitu vingi mbalimbali ambao waliletwa na Wizara.

” Sasa hapa tuna Madini yanayotupwa, kule wanaofanya uchechuaji wanakamata zaidi Dhahabu na Silva, maana Silva nyingรญ inabaki kwenye tope, waje na Teknolojia ya kukamata silva inayobaki kwenye tope, kwasababu sokoni tunahitaji Silva lakini sio kwa mchimbaji, mchimbaji anatafuta dhahabu kwa hiyo asilimia anayopatikana baada ya kuchenjuliwa ni ile ambayo imekamatwa Kwa bahati mbaya.

Aidha ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na Teknolojia ya kuanza kukamata Silva, dhahabu, yakamatwe na Madini mengine ili tusitupe utajiri huu kwenye matope na Madini mengine kama hapa walivyokuja hapa watu wanaochimba madini ya vito ( Tanzanite) kutoka Mirerani tumefurahi sana, kwasababu na Geita yapo mawe aina hii ambayo yanaweza kufanyiwa nakshi watu wakanunua wakavaa, wakaacha kuvaa maplastiki.

Naye mfanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Tanzanite ya Franone Mining & Gems Company Ltd Furaha Mshai amesema ujio wao kwenye Maonyesho hayo ni fursa pekee ya kutangaza Madini yao aina ya Tanzanite na kuwaonyesha Watanzania Madini pekee yanayopatikana hapa nchini ambayo ni Tanzania.

Mshai amesema Madini hayo yamekua ni kivutio kikubwa katika Maonesho hayo na kama mavyofahamu Madini ya Tanzanite yanapatikakana Wilaya ya Simanjiro mkoa wa manyara nchini Tanzania kwa maana hiyo ni Tanzania tu ndio tunachimba Tanzanite

Tunapaswa kumshukuru MUNGU kwa kuipendelea nchi yetu kwa kuweka mali adimu na utajiri mkubwa unaopatikana Tanzania Amesema Mshai.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram