188 views 55 secs 0 comments

SERIKALI KUONGEZEA WIGO SEKTA YA MAWASILIANO

In BIASHARA, KITAIFA, MICHEZO
September 25, 2023

Wizara ya Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa kuweka mazingira wezeshi kwa makampuni ya kutoa huduma ya mawasiliano ili kuongeza wigo katika sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa leo septemba 25,2023 na Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape nnauye kwenye Hafla ya utiaji saini hati ya maridhiano na hati ya mkataba wa nyongeza kwenye miundombinu ya mkongo wa mawasiliano, jijini Dar es salam.

Hatua hiyo imekuja kufatia Maelekezo kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekeza kutatuliwa Kwa migogoro uliokuwepo kati ya umoja huo na serikali jambo lililosababisha kukwama Kwa shughuli za uwekezaji ili sekta kuwa wezeshi na kuchangia uchumi wa Taifa.

“Kwa kutambua umuhimu wa Tehama Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi Kwa watoa huduma na wawekezaji kujenga miundombinu ya Mawasiliano kote Nchini na wakahakikishia tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha”Amesema Nnauye


Aidha, Mhe. Nape ameyataka makampuni ya kutoa huduma za mawasiliano kuwekeza zaidi kwenye miundombinu ili kufikia wananchi wengi zaidi pamoja na kusihi mikataba hiyo izingatie utekelezaji na kuonesha matokeo endapo itatokea uzembe basi hatua zichukuliwe mapema kabla ya kufikia migogoro.

Akieleza miongoni mwa juhudi za serikali Katika mawasiliano imepunguza gharama za kuweka miundombinu ya mkongo kutoka Sh.2.5 Milioni Hadi Sh.250.000 lakini pia inaendelea na ujenzi wa mkongo wa Taifa ambao unatarajia kuzifikia wilaya 99 kati 139 ifikapo machi 2024 huku lengo likiwa kufikia wilaya zote ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram