253 views 49 secs 0 comments

TAMISEMI KUSAINI MKATABA WA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI

In KITAIFA
September 23, 2023
Utiaji saini mkataba wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya miji ya Tanzania TACTIC

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mh.Mohamed Omary Mchengerwa ameshuhudia utoaji saini wa mkataba wa miradi wa uboreshaji wa miundombinu ya miji ya Tanzania uliofanyika septemba 23 katika ukumbi wa JNICC jijini dar es salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo waziri Mchengerwa amesema mkataba huo ni wa dola mil 110 ambazo ni zaidi ya shilingi Til1 zitakazohudumia miradi katika miji 45.

Aidha waziri Mchengerwa amewataka wakandarasi wahakikishe wanamaliza miradi kwa wakati na ubora uliopangwa kwasababu hakutakua na muda wa ziadi katika miradi hiyo

Vilevile amewataka Tarura kuhakikisha fidia za waathirika wa miradi inafanyika mapema pamoja na kusimamia miradi yote.



Hata hivyo waziri Mchengerwa amewataka wakurugenzi kuhakikisha fedha zote za miradi zinakwendwa kutekeleza miradi nakuongeza kuwa mkurugenzi yeyote ataenda tofauti atamsimamisha kazi.

“Atakaye nivuta shati nitakuvuta shati kwanza sitakubali hata kidogo” alisema waziri Mchengerwa

“Kampuni hiyo imepewa kazi ya ujenzi wa daraja na barabara kwenye halmashauri hiyo na fedha wameshalipwa lakini mpaka Sasa kazi hiyo hawajaanza hivyo baada ya kazi ya Leo ya TACTIC wasipewe kazi wengine mpaka wamalize kazi hizo”Aliongezea Mchengerwa

Aidha mchengerwa amesema mradi huu wa TACTIC unatekelezwa Katika Halmashauri 45 Nchini na uasimamiwa na Ofisi ya Rais-Tamisemi Kupitia wakala wa barabara za VIJIJINI na mijini (TARURA) na itagharimu Dola za kimarekani MILIONI 110

Madina Mohammed

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram