231 views 3 mins 0 comments

BOT KUNUNUA DHAHABU KWA AJILI YA KUTUNZA AKIBA ZA NCHI

In KITAIFA
September 23, 2023


GAVANA wa Benki Kuu (BoT) Emmanuel Tutuba amesema,moja ya majukumu ya Benki hiyo ni pamoja na kushiriki katika masuala ya uchumi ambapo hununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha.

Tutuba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BoT kwenye maonesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya Madini mkoani Geita kwenye viwanja vya EPZA vilivyopo Bombambili halimashauri ya mji wa Geita
Amesema lengo la kununua dhahabu na kuziuza nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na hivyo kuwezesha kusapoti uchumi wan chi.


“Kwa hiyo ushiriki wetu katika masuala ya kiuchumi ni pamoja na kununua dhahabu ikiwa ni namna mbadala ya kuendelea kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha taslimu lakini pia tunanunua dhahabu ili tupate fedha za kigeni baada ya kuuza nje na fedha ziweze kusapoti uchumi wa nchi.”amesema Tutuba.


Akizungumzia kuhusu kuadimika kwa dola Tutuba amesema,changamoto hiyo ni kutokana na kuadimika kwa dola kwenye mzunguko wa uchumi kidunia .
Hata hivyo amesema,pamoja na changamoto hiyo BoT bado ina dola za kutosha kugharamia shughuli za kiserikali pamoja na shughuli za kipaumbele kwa wakati huo.


“Hii ni kutokana na ‘reserves’ ya Dola ilitunzwa na BoT, lakini sasa watu wengine wanachanganya, wakisikia reserves za nchi wanadhani ni fedha ambayo ya kuwagawia watu ,lakini kimsingi hizi reserves ndio zinasaidia nchi katika kipindi kama hiki ambacho dola imeadimika.”amesisitiza Tutuba na kuongeza kuwa


“Kwa hapa tunaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya serikali kwa kuwa tunayo fedha ya kutosha kutekeleza miradi malimbali kwa mwaka mzima lakini hata pakitokea hatari na mipaka ikifungwa zile fedha tunaweza kuzitumia kwa mwaka mzima.

Gavana Tutuba ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais DKT.Samia Suluhu Hassan kwa Filamu yake ya Royal Tour ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza Dola kutokana na watalii wengi kuja kutalii hapa nchini.

“Kwa hiyo katika mzunguko kitakwimu dola inaendelea kuongezeka na hivyo kuondoa kikwazo cha kuzuia uchumi uendelee.”


Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho hayo amesema,wameshiriki kikamilifu kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau wanaohitaji kujua namna BoT inavyoshiriki kwenye sekta ya madini.


Aidha amesema ,BoT ina dhamana ya kusimamia masuala ya ukuaji wa uchumi na uhimilivu wa bei pamoja na mzunguko na thamani ya fedha .


“Sisi tumefika katika maonesho haya ikiwa ni mojawapo ya mikakati yetu ya kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi kwa ujumla kuhusu BoT na kushiriki katika masuala ya ukuaji wa uchumi.”amesisitiza Gavana huyo

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram