288 views 3 mins 0 comments

TMDA CHANGAMOTO YAKITHILI UHABA WA WATAALAMU MAABARA

In KITAIFA
September 22, 2023

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Tanzania pamoja na kuwa kati ya nchi nne zenye mfumo wa maabara ulitengenezwa Kwa matakwa ya nchi husika,lakini inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu wa Uchunguzi Katika maabara.

Hayo yalibainishwa na mkurugenzi wa huduma za maabara wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Dk Danstan shewiyo wakati wa kikao kazi Cha TMDA na wahandishi wa habari,mkoani Dar es salaam



Dk shewiyo Alisema pamoja na juhudi za serikali kuhakikisha inalinda Afya za watanzania lakini kumekuwa na changamoto ya wataalamu mbalimbali wa maabara.

Alisema mbali na uhaba wa wataalamu wa Uchunguzi wa maabara,pia hakuna wataalamu wa kutosha kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa sampuli mbalimbali na mara nyingine kulazimika kutumia wataalamu kutoka Bara la Asia,Ulaya na Ujerumani.



Alitoa wito Kwa serikali kuweka mazingira wezeshi ya kufundisha wataalamu wengi Zaidi Katika vyuo hapa nchini Ili waweze kupatikana Kwa wingi

Dkt shewiyo alibainisha pia Kuna changamoto ya mahitaji mengi ya maabara kutopatikana kirahisi hapa nchini,na hivyo kulazimika kutafuta mahitaji hayo nje kama kwenye nchi za Afrika kusini,India,Ulaya na Bara la Asia na vinapoagizwa huko huchukua Muda mrefu kufika.



Hata hivyo,Alisema pamoja na changamoto hizo zote Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa zenye maabara zinazotambulika Kwa ufanisi na imekuwa kimbilio la nchi mbalimbali za Afrika

Akizungumzia Zaidi ufanisi wa TMDA Kwa upande wa maabara,Alisema mamlaka hiyo ilikuwa na maabara za kuhamishika 25 na imepokea maabara nyingine mbili kutoka jumuiya ya Afrika mashariki EAC na kufanya Sasa kuwa na jumla ya maabara za kuhamishika 27 ambazo ziko Katika maeneo mbalimbali hivyo kuiwezesha mamlaka hiyo kufanya kazi zake Kwa ufanisi



Dk shewiyo Alisema,kutokana na uwezo wa maabara kubwa ya TMDA Kuna baadhi ya nchi zimekuwa zikileta watu wake kuja kujifunza ikiwemo Malawi,Zambia Botswana na Rwanda

Alitaja pia baadhi ya nchi ambazo zimekuwa zikileta sampuli zake Kwa ajili ya kupimiwa Katika maabara ya mamlaka hiyo kuwa ni pamoja msumbiji,Libelia,Gambia,Lesotho na Burundi



Katika hatua nyingine kaimu mkurugenzi wa dawa za binadamu na mifugo Emmanuel Alphonce Akitoa mada Kuhusu mchango wa TMDA Katika kutekeleza sera ya viwanda Alisema Hadi kufika mwaka 2017, Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 13 lakini Sasa Kuna jumla ya viwanda 17 na kati ya viwanda hivyo 11 vinajihusisha na kuzalisha dawa za binadamu na sita dawa za mifugo.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram