

Ofisi ya mkuu wa wilaya Kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato TRA imeshirikiana kuandaa week ya EFD ambayo inayotumika Kwa kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine ya EFD kwa wafanyabiashara
Ili Kujenga mahusiano mazuri kati ya walipa kodi na wafanyabiashara wa Ilala na TRA na serikali imekuwa ndo kiunganishi Cha kujenga mahusiano hayo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo Jumatano 20 September 2023 Mkuu wa wilaya ya Ilala Endward Mpogolo amesema week hii ya EFD ambayo itakuwa tarehe 23 kutakuwa na Kuna fun marathon ya kilomita 10 na 5
“Tuko Katika hatua ya mwisho ya kukamilisha upatikanaji wa medani,Kidisi,na maandalizi ya luti.na maandalizi yote ya marathon yameshafanyika na tunategemea kuwa na washindi watano Kwa kila eneo.la kilo meta 5 na 10 Kwa wanawake na wanaume ambao watakao shinda watapatiwa zawadi “amesema Mpogolo
Aidha Amesisitiza kuwa watu waendelee kujisajili Katika website ya TRA Kwa kujisajili kushiriki watembelee website hiyo Kwa kujiunga na wale watu wa mwanzo ambao watakaojiunga watapata jezi mpya Na Kauli mbiu ya siku ya week ya EFD Marathon ni RISITI YAKO NI ULIZI WAKO
Aidha Mpogolo amesema Katika mbio hizo za kilomita kumi zitaazia Katika viwanja vya jakaya na kumalizia Katika viwanja hivyo vya jakaya Kwa kilo meta 5 na 10
Katika week hiyo ya EFD na mashindano hayo ya marathon mgeni rasmi atakuwa mkuu wa MKOA wa dar es salaam Albert chalamila na watu Zaidi ya elfu 2 watashiriki na taasisi pia zimeonyesha muelekeo wa kushiriki ni Zaidi ya 600

MADINA MOHAMMED