
Kampuni ishirini na tano (25) zilizopewa nyaraka za zabuni Kupitia mfumo wa ununuzi serikalini (TANePS) ambazo kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za zabuni
Jumla ya kampuni tano zimetia saini makubaliano ya uchimbaji wa makaa ya mawe Katika mradi wa mchuchuma ambayo mikataba hiyo itadumu Kwa Muda wa miaka mitano
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri wa viwanda na biashara Dkt.Ashatu Kijazi amesema zoezi la ulipaji fidia umefanyika Kwa mafanikio na watu 25 kati ya wafidiwa 1142 ndio hawajapokea fidia kutokana na kutojitokeza Ili kujaza nyaraka za malipo
Aidha makampuni haya yanatarajia kuanza rasmi shughuli za utafiti mnamo mwezi Oktoba 2023 Na uchimbaji mara baada ya kukamilisha utafiti
“Wakati zoezi la ulipaji wa fidia likifikia tamati Katika historia ya nchi yetu tunashuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba na wachimbaji wazawa ambapo kama tulivyojulishwa ni kuwa jumla ya mikataba mitano itasainiwa”. Amesema Dkt Kijazi
“Dhamira ya dhati na ya hali ya juu ya serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha ndoto za Utekelezaji wa mradi wa liganga na mchuchuma zinafika mwisho na rasilimali hizi ambazo zimekaa kwa Muda mrefu bila kuwanufaisha wananchi ziwanufaishe na kuchangia Katika uchumi wa nchi”. Aliongezea Dkt Kijazi
Nae Mwekezaji wa madini Ndaesaba amesema shirika la maendeleo linatekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo mradi wa chuma Cha liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma iliyopo Katika wilaya ya ludewa,mkoa wa njombe,
“miradi hii inatekelezwa Kwa pamoja na kampuni ya Sichuan Hongda Group (SHG) ya china Kupitia kampuni ya ubia inayoitwa Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) ambayo serikali inamiliki asilimia 20 na SHG asilimia 80”, Amesema Ndaesaba
Aidha Ndaesaba amesema Serikali Kwa kutumia Timu ya majadiliano GNT inafanya majadiliano na imeshalipa fidia na Utekelezaji wa miradi hii unatarajiwa kuendelea mara baada ya kukamilika majadiliano mwishoni mwaka huu



MADINA MOHAMMED