Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya mifumo ya chakula (AGRA) na kampuni ya John Deer inatarajia kuanza mchakato wa kuwashindanisha vijana kwenye vikundi na kuwapatia zawadi ya trekta lengo likiwa kuendelea kuhamasisha vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema WAKATI Akipokea trekta lililokabidhiwa kwa Serikali kutoka kampuni ya Kimataifa ya wauzaji wa matrekta ya JOHN DEERE, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema ili kuwakabidhi vijana trekta hilo umeandaliwa utaratibu wa kutangaza mashindano ili kumpata mshindi.
Bashe ameeleza kuwa utaratibu huo wa kumpata mshindi utahusisha mashindano ya vikundi vya vijana ambavyo vitatakiwa kuwasilisha andiko la wazo la biashara wanayotaka kufanya katika sekta ya Kilimo kuendana na matumizi na uhitaji wa trekta hilo.
โMchakato huo utakuwa transparent tutashirikiana na Johndear, wizara ya Kilimo na AGRA kwa ajili ya kuendesha hayo…..Kikundi cha vijana kitakachoshinda kitakabidhiwa trekta”. Amesema Waziri Bashe
Makabidhiano ya trekta hilo yamefanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam unapofanyika mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF).