Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka watendaji wa ofisi yake kutangaza mafanikio ya wizara na taasisi zake ili wananchi waweze kutambua fursa zinazo wezeshwa na serikali.
Mhandisi Luhemeja amesema hayo Septemba 7, 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili shughuli na kazi za Wizara na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo, kilichofanyika jijini Dodoma.
Amesema ni muhimu kutumia vyombo vya habari kuzungumzia namna ofisi hiyo inavyo ratibu, kusimamia na kukuza sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ustawi wa Watu Wenye Ulemavu.
Aidha ameshauri pia ziandaliwe programu maalum kupitia vipindi vya elimu kwa umma vitakavyo elimisha wananchi kuhusu fursa pamoja na majukumu mengine muhimu yanayotekelezwa na serikali kupitia ofisi hiyo.
Kwa upande wake Mchoraji katuni na Mdau wa Vijana, Ali Masoud (Kipanya) amesema yupo tayari kushirikiana na ofisi hiyo kutangaza mafanikio yanayofanywa na serikali katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini.