Tanzania na Uganda inaendelea kuimarisha ushirikiano na mahusiano katika sekta ya mifugo kwa kusaini makubaliano ya udhibiti wa magonjwa ya wanyama yanayovuka mipaka na yanayo ambukiza binadam katika maeneo ya mipaka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo Alhamis 07 September 2023 Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Hamis Ulega Amesema Licha ya uwepo wa mifugo mingi Nchini bado sekta hiyo inamchango mdogo katika uchumi wa Nchi takriban asilimia saba (7%) ya pato hutoka kwenye mifugo, na imebainika kuwa sababu kubwa ya kutofanya vizuri kwa sekta hiyo ni magonjwa ya mifugo.
“ sisi Tanzania tuna mifugo mingi tunazo ng’ombe takriban milioni 36, tunao mbuzi takriban milioni 26, tunao kondoo milioni 9 na kuku wale wakienyeji na wakisasa takriban milioni 97, nguruwe milion 3, pamoja na uwepo wa mifugo hiyo mingi lakini bado tunaona mchango wa sekta ya mifugo ya Nchi yetu ni mdogo ni takriban asilimia saba (7%) ya uchumi wa Taifa letu, Tafiti zinaonyesha wazi kuwa pamoja na sababu zingine lakini moja ya sababu kubwa kabisa ni uwepo wa magonjwa ya mifugo katika hayo magonjwa ya mifugo ni pamoja na magonjwa yenye kuhama” amesema Mhe. Ulega
Aidha makubaliano hayo yanatokana na mpango wa muda mrefu wa Serikali hizo mbili yaliotokana na mazungumzo ya baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni na hivyo kuona kuna umuhim wa kuwepo mikakati ya kudhibiti magonjwa hayo.
Naye Waziri wa Nchi anaye shughulikia sekta ya mifugo wa Uganda Mhe. Bright Rwamirama amezungumzia uwepo wa uhusiano wa asili uliyopo baina ya Tanzania na Uganda ni kutokana na ukaribu wa Nchi hizi mbili na kusema kuwa Mataifa haya mawili yaliweza kutenganishwa kwa mipaka ya Nchi lakini bado Magonjwa yanaendelea kuvuka mipaka hivyo ni lazima kuwepo na mipango ya makusudi ya kudhibiti Magonjwa.