195 views 2 mins 0 comments

RAIS SAMIA MPANGO WA BBT NI KUSHUSHA MFUMUKO WA BEI YA CHAKULA

In KITAIFA
September 07, 2023

Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Kupitia serikali yake wataambatanisha viashiria na vitaashiria kufanikiwa Kwa mpango wa kilimo wa BBT Ili kuwapatia fursa Vijana kujihusisha na Kilimo.

Amesema kuwa na kutaja baadhi ya viashiria hivyo ni idadi ya Vijana walio Katika mpango huo ambao wapo Zaidi 1200 Na Bado wapo Katika Kasi ya uhitaji

“viashiria hivyo ni kuvutika na Vijana Kwa mpango kazi wa BBT na kipengere chengine ni wanavyotumia mbolea Katika uzalishaji na inavyotumika na kuelewa kuwa Vijana wameelewa na wanafanya kilimo Cha kisasa”.Amesema Rais Samia

Hata hivyo Rais Samia amesema kiashiria kingine ni soko Kwa maana Vijana watakapopeleka mazao sokoni wataendesha maisha Yao na kikubwa napenda kuona maisha ya Vijana yanavyoweza kustawi

Aidha Rais Samia amesema kuwa Serikali imejizatiti kujenga barabara za kuunganisha Mikoa na Wilaya zake mpaka nchi jirani ili kuongeza masoko kwa wakulima na kuepukana na vikwazo

Hayo Yamesemwa Leo Alhamis 07 September 2023 jijini Dar es salaam na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na vijana mbalimbali katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF) ambapo amesema kuwa Serikali imejenga barabara za ndani Ili mazao ya wakulima yasikwame katika maeneo mbalimbali.

Rais Samia amesema kuwa kuhusu kutumia Tehama wamewekeza katika ufanyaji wa tafiti kwenye Kilimo na Uvuvi Ili kujua afya ya udongo,aina ya wakulima sambamba na kufahamu Kilimo wanachokifanya.

Ameongeza pia kufanikiwa kwa mpango wa BBT ni pale watakapoona wameshusha mfumuko wa bei ya gharama za chakula ndani ya nchi.

“Kama uzalishaji utakuwa mkubwa bila shaka bei za chakula zitashuka na kama tunavyojua mfumuko ndio unasababisha bei za chakula kupanda ndani ya nchi.
Tukiweza kushusha mfumuko wa bei ya vyakula kitakuwa kiashiria kizuri sana kwamba vijana wanazalisha kwa wingi.”

Madina Mohammed

/ Published posts: 1487

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram