Mpango wa Serikali wa kuwatoa Watanzania kutoka kwenye umaskini kupitia kilimo unaonekana dhahiri kutokana na hatua mbali mbali inazochukuliwa kuboresha sekta hiyo.
Aidha miongoni mwa hatua madhubuti za kuimarisha sekta hiyo ni pamoja ni kuongezeka kwa bajeti ya kilimo hadi bilioni 970 kwa mwaka huu, fedha hizo zimelenga kufanya mageuzi kutoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua na kujikita kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumatano 06 September 2023 Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) Serikali imetenga zaidi ya Bilioni 370 kwa ajili ya kujenga mabwawa na kuchimba visima pamoja na kuboresha miradi ya umwagiliaji ili wakulima waweze kuzalisha mazao mwaka mzima.
โSerikali imetenga zaidi ya bilioni 370 kwajili ya kujenga mabwawa, kuchimba visima kwajili ya kuweka miradi ya umwagiliaji vizuri wakulima waweze kuzalisha mazao mwaka mzima badala ya kutegemea mvuaโ amesema Msigwa
Pia lengo la Serikali ni kuongeza hifadhi ya chakula katika maghala ya chakula Nchini, kwasasa maghala yanayo jengwa yanafikia tani 501,000 na mpango uliopo ni kutanua zaidi ili kufikia uwezo wa kuhifadhi tani 750,000 mwaka 2025.
Aidha Msigwa amesema kesho ni siku ya Marais kukutana Katika mkutano huo wa jukwaa la mfumo ya chakula Afrika AGRF 2023 ambapo watakutana Marais mbalimbali na kupokelewa na mwenyeji wao Rais Samia Suluhu Hassan
MADINA MOHAMMED