217 views 2 mins 0 comments

WAZIRI ULEGA: WAWEKEZAJI WANAPASWA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UVUVI

In KITAIFA
September 05, 2023

SERIKALI imeweka mikakati itakayotekelezwa na nchi hivyo kuwa kitovu cha chakula Afrika na duniani kote,ili iweze kunufaika na tishio la baa la njaa linaloikabili dunia,kwa kuuza chakula katika maeneo mbalimbali
duniani.

Mikakati hiyo ni pamoja na ile ya Kibajeti,Kisera,Teknolojia,Uwekezaji
na Ushirikiano baina yake na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya
nchi.

Hayo yanatokea wakati takwimu zinaonyesha wananchi barani Afrika
watakaokabiliwa na upungufu wa chakula wataongezeka na kusababisha
kiasi cha fedha za kigeni zitakazotumika kuagiza chakula kuongeza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumanne 05 2023 Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere JINCC Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amebainisha hayo wakati wakiwa Katika
mkutano wa mifumo ya chakula Afrika (AGRF),uliojumuisha watu 5,000
kutoka mataifa 70 Duniani.

Ulega Amesema serikali wamejipanga kuhakikisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi zinapiga hatua Ili kuleta tija.nchini ambapo wanachangamoto ya mazao Kwa asilimia 70 yanayotokana na kilimo na teknolojia, uwekezaji,mitaji na masoko Ili waweze kuvutia wakina mama na Vijana

“Tunahitaji mitaji Ili Vijana waweze kuingia na tunahitaji digital teknolojia Ili wafanye biashara Kwa njia ya kidigitali na tunahitaji teknolojia ya kisasa Ili waweze kuwavuta wakina mama na Vijana kwani wao ndio Asilimia kubwa Kwa watu tuliokuwa nao na soko lipo kubwa sana ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu”Amesema Waziri Ulega

Sekta ya kilimo imejipanga na fursa kubwa ambazo tulizozieka Katika nchi yetu na milango imefunguka vizuri,Kuna kilimo mazao, kilimo mifugo na kilimo uvuvi vyote hivyo vinategemeana Katika uzalishaji

Ulega amesema ili kuboresha sekta ya kilimo,uvuvi na mifugo teknolojia,masoko na mitaji inahitajika hivyo wawekezaji wanapaswa kuwekeza ili kukuza sekta hiyo ili kuzalisha kwa tija na kuuza nje.

Mkutano wa mifumo ya chakula Afrika AGRF unafanyika jijini Dar es salaam ambapo unahudhuriwa na watu zaidi ya 3000 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika..

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram