281 views 3 mins 0 comments

WAZIRI BASHE: TANZANIA KUONGEZA HEKARI MILION 8 SUALA LA KILIMO

In KITAIFA
September 05, 2023
Viongozi mbalimbali na wadau wakiwa Katika presentation ya waziri wa kilimo Hussein Bashe

Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema Tanzania inahitaji kiasi Cha fedha zaidi ya Tilioni 1.3 Kwa mwaka ifikapo 2025 ili Nchi ifikie lengo la kuongeza hekari milion 8 Katika masuala mbalimbali ya Kilimo.

Hayo yamejiri Jijini Dar es salaam Katika kikao Cha ufunguzi wa Jukwaa la Mfumo WA Chakula Afrikan AGRF 2023 kilichowakutanisha Mawaziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka bara na visiwani na wadau wa Sekta ya kilimo Ili kuzungumzia Sekta hiyo na kutoa fursa Kwa wawekezaji kuja kuwekeza Nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wanamikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha Mradi wa kilimo Cha umwagiliaji kinakachogharimu zaidi ya Dola million mia tatu sambamba na Mradi wa Afrikan Development utakao gharimu Dola million moja Kwa ajili ya Kilimo Cha Vijana Nchini ambapo utekelezaji wake utaanza januar 2024.

“matumizi kama nchi tumeanza kupromoti kilimo Cha mihogo Kwa kulitanganza soko la China na serikali inadizaini mikakati Kwa sababu matumizi ya mihogo sio tu Kwa ajili ya kupeleka china hata sisi ndani ya nchi yetu tuna viwanda vinavyotumia mihogo”Amesema Bashe


Kwa upande wake Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema wamejipanga kuhakikisha Sekta ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi zinapiga hatua ili kuleta tija Nchini mbapo wanachangamoto ya mazao kwa asilimia 70 yanayotokana na Kilimo na teknolojia, Uwekezaji ,mitaji na masoko ili waweze kuwavutia akina mama na Vijana.

“Tunaitaji mitaji Ili Vijana waweze kuingia na tunahitaji digital teknolojia Ili wafanye biashara kwaa kidigitali na tunahitaji teknolojia ya kisasa Ili waweze kuvuta wakina mama na Vijana kwani wao ndio asilimia kubwa Kwa watu tuliokuwa nao na soko lipo kubwa sana la ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu”Amesema Ulega


Nae Waziri wa fedha Uchumi na Mipango Mwigulu Nchemba amesema Azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuwekeza Katika Sekta ya uzalishaji na kupeleka nguvu kazi iwe kazini.

“Tunahitaji kuzalisha soko la mayai tule wenyewe na tuwapelekee hata nje ya nchi Kwa mfano mahali kama nchi kama somalia inauhaba wa chakula tukiwapelekea chakula na mayai ambayo teali yameshachemshwa kabisa na kupeji itatuongezea uwekezaji Katika nchi yetu ya Tanzania”Amesema Nchemba

MADINA MOHAMMED

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram