303 views 1 sec 0 comments

KANYE WEST NA MKE WAKE WAPIGWA ZUIO LA MAISHA.

In BURUDANI
September 04, 2023

Rapa na Mfanyabiashara wa Marekani, Kanye West na mkewe, Bianca Censori, wamepigwa zuio la maisha na Kampuni maarufu ya kukodisha Boti ya Venezia Turismo Motoscafi, baada ya wanandoa hao kunaswa katika picha wakishiriki matendo ya ngono kwenye moja ya Boti ya kampuni hiyo. Huku sehemu ndogo ya makalio ya Ye ikiwa wazi.

Kampuni hiyo yenye maskani yake Tronchetto, Italia imelaani vikali kitendo hicho kilichosababisha mshtuko mkubwa kwa jamii kufuatia picha chafu zilizosambaa mitandaoni wakiwa katika safari yao hiyo ya Boti nchini Italia hivi karibuni.

Katika taarifa ilitolewa na Venezia inaeleza kuwa hawata wakaribisha tena Kanye na Bianca kwenye Boti zao.

Mwezi uliopita Wakazi wa Italia, walionesha kukerwa na uvaaji wa Bianca Censori, mke wa Kanye West na
kuwataka kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram