
Chama Cha ACT wazalendo kinaunga mkono Uwekezaji WA Bandari ya Dar es salaam kati ya Serikali ya Tanzania Na Dubai DPWorld ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi wa Bandari hio
Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Dorothy Semu alipokitana na Waandishi WA Habari Kwa lengo la kutia ufafanuzi kuhusu Uwekezaji WA Bandari hiyo unaotekekezwa hapa Nchini.
Semu amesema japokua wanaunga mkono Uwekezaji huo lakini Chama kimebaini mapungufu mbalimbali ikiwemo kutowashirikisha Wananchi na Makampuni Katika Uwekezaji sambambamba na Jamii Elimu kuhusu DP World ili kuondoka Sinto fahamu zinazojitokeza hapa Nchini.
Aidha amesema wanakubalinana kuwa Bandari zetu hazina ufanisi mzuri hivyo zinahitajika jitihada mbalimbali za kuongeza ufanisi na tija ili Nchi iweze kunufaika na ukuaji WA uchumi Kwa kutumia bandari
MADINA MOHAMMED