537 views 45 secs 0 comments

MBASHA ATAMBULISHA WASANII WAPYA WA INJILI

In BURUDANI
August 30, 2023
Emmanuel Mbasha akiwatambulisha wasanii hao mapacha Katika waandishi wa habari

Msanii wa muziki wa injili hapa nchini,Emanuel Mbasha amewatambulisha rasmi wasanii wapya wa muziki wa injili ambao wanaitwa Mapacha wa Mungu kama sehemu ya project yake ya Mbasha House of talent.

Mbasha amesema ujio wa wasanii hao mapacha kwenye muziki wa injili utakwenda kutikisa tasnia ya Muziki wa injili hapa nchini kwa kuongeza ladha mpya ya muziki huo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katika hotel ya center point wakati wa utambulisho rasmi wa wasanii hao,Mbasha amesema ameamua kuibua vipaji vya vijana hao ikiwa ni sehemu ya kuonyesha jitihada zake kama mlezi wa muziki wa injili Tanzania.

Amesema kuwa mapacha wa Mungu ni wasanii wenye vipaji vikubwa vya uimbaji hivyo watanzania wanapaswa kuwapokea kwa mikono miwili ili kuendelea kulisongesha gurudumu la muziki huo pendwa kwa sasa nchini.

Aidha kwa upande wao wasanii hao ‘pacha’ mapacha wa Mungu wamesema wameamua kutumia vipaji vyao kwa kumtumikia Mungu kupitia muziki wa injili hivyo wamewaomba wapenzi na mashabiki wa injili
nchini kuwapokea.

“tunamshukuru sana kaka Mbasha na menejiment yetu kwa kutusaidia kufika hapa tulipo na tayari tumetambulisha wimbo wetu mpya uitwao Only you ambao unapatikana kwenye mitandao yote ya kidigitali ya kimuziki(digital platforms) zote duniani”amesema pacha

Madina Mohammed

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram