
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji kwa kina askari wa kampuni ya ulinzi PASCO LTD 11, Maafisa wakala Huduma za misitu (TFS) wawili na askari Polisi 6.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Leo tarehe 29 agosti 2023 Katika ofisi za makao makuu polisi post kamanda wa polisi Kanda maarum ya Dar es salaam Muliro Jumanne Murilo amesema Kushikiliwa kwa watu hao kunatokana na tuhuma za kujeruhiwa kwa watu wawili ambao baadae walipoteza maisha na suala hili lipo Katika uchunguzi wake na tayari uchungunzi unaendelea kufanyika.
“Tarehe 28 Agosti, 2023 Majira ya saa 8 usiku eneo la Kiluvya Ubungo, maafisa kutoka katika taasisi hizo wanadai wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, lilitokea kundi la watu wanaokadiriwa kuwa 30 wakiwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba magunia ya mkaa ambayo ni mazao ya misitu na walipofika eneo la ukaguzi na kuamriwa wasimame, walikaidi na kuanza kufanya fujo kubwa kwa kuwarushia mawe Maofisa wa maliasili na wenzao wakishinikiza pikipiki zilizo kuwa na mkaa kinyume na sheria ziachiwe”. Amesema Muliro
Katika hatua nyingine Muliro amesema kuwa Mafisa wa team hiyo waliokuwa na silaha walianza kufyatua risasi kwa lengo la kuwatawanya na kujilinda. Hata hivyo ilibainika watu wawili walijeruhiwa katika purukushani hizo na walipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali ya Mloganzila.
“Katika tukio hilo Pikipiki 16 ambazo zilitelekezwa na watu hao na magunia ya mkaa vilipelekwa Mpingo house. Jeshi la Polisi Kanda Maalum linachunguza mazingira yote ya tukio hili kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kisheria na halitasita kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua zingine za kisheria kulingana na sheria za Nchi”Aliongezea Muliro
Aidha Muliro ameongeza Kwa kusema kuwa Watu waliokuwa kwenye kazi hiyo wako chini ya ulinzi na silaha zao zimepelekwa kwenye mamlaka za kiuchunguzi za silaha /bunduki
Pia Muliro amesema Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi Zaidi.
Madina Mohammed