MKURUGENZI wa kampuni ya vifaa vya ujenzi ya SHEVA HARDWARE MaryStella Temba amewaasa wachimbaji wadogo kutumia vifaa vya usalama sehemu za migodi kwa kufanya hivyo watakuwa salama.
Amesema kuwa wamekuwa kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wamegundua kuwa iko haja ya wachimbaji wadogo kutumia vifaa bora haswa kutoka kwao kwasababubu vinaubora wa hali ya juu na vinagaratiii.
kauli hiyo imetolewa Leo Agosti 24 na mkurugenzi wa kampuni ya Sheva Hardware MaryStella Temba katika maonyesho ya madini ambayo yanafanyika wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.
amesema kuwa wao kama Sheva Hardware wanawakaribisha wananchi kwenye Banda la Kampuni hiyo Ili kuona na kupata vifaa mbalimbali vikiwemo vya kwenye migodi.
“Sheva Hardware ni Kampuni ya kitanzania ambayo imejipambanua kuuza na kusambaza vifaa mbalimbali ikiwa pamoja na majembe,sululu, kofia ngumu, viatu ,Nondo, na vinginevyo.”amesema Merystella
Nakuongeza kuwa ” sisi kama Hardware tumejipanga vizuri sana kuhakikisha tunatoa huduma Bora na sahihi kwa watanzania na nivema kutumia maonyesho haya ya madini ambayo yanafanyika hapa Ruangwa kuhakikisha wananchi wanakuja kupata kilichobora.”amesisitiza Merystella.
Amesema kuwa “tumeanza na mkoa wa Lindi kwasababubu ni mkoa ambao unasemekana una madini ya aina nyingi hapa nchini kuliko mikoa yote kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na tume ya madini.
Merystella ameongeza kuwa anawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao lililopo ndani ya viwanja vya soko jipya kilima hewa kujionea vifaa vya ujenzi vyenye ubora na kupata bei nafuu kuliko mahala pangine popote pale.
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa wameanza na mikoa miwili ambapo ni Dar es laam na Lindi wilaya ya Ruangwa tunawakaribisha wote kuja kupata ushauri wa bure kabla hawajaanza ujenzi sisi tutakushari namna ya kufanya kwenye ujenzi”, amesema Temba