
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa basihaya ndugu Samson Andrew amekabidhi jezi kwa washiriki wa michuano ya adrew supa cup inayofanyika kata ya basihaya bunju jijini dar es salaam
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akigawa jezi hizo ndugu Samsoni amesema wanamtarajia mbunge wa kawe ndugu Josephat Gwajima kuwa mgeni rasmi kwenye fainali hizo ambazo zitachezwa hapo kesho
Mshindi wa kwanza katika fainali hizo kwa upande wa mpira wa miguu ataondoka na kitita cha sh millioni moja akifuatiwa na mshindi wa pili shilingi laki tano
Kwa upande wa rede mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja hukushindi wa pili alijipatia shilingi laki tano
Aidha mwenyekiti ameweka wazi lengo la kuanzisha mashindano haya kwa kuwataka wananchi wa basihaya kufanya mazoezi lakini pia kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi
“Atujabagua mtu watu ,wananchi wote wameshiriki michuano hivi sio wa chama cha mapinduzi tu”alisema mwenyekiti
Vilevile aliwataka wananchi wote kuhudhuria mashindano hayo kwani kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwemo wa singeli