350 views 15 secs 0 comments

RAPID: SERIKALI IWEKE KANUNI NA SHERIA ILI KUKABILIANA NA MAJANGA NA MAAFA

In KITAIFA
August 23, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Watoji huduma ya majanga na maaafa nchini watoe Elimu mashuleni na katika vikundi ili kuepukana na majanga mbalimbali yasiendelee kujitokeza Nchini.

Wito huo umetolewa katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya kuwaenzi watoaji huduma hiyo Duniani ambapo Chalamila amewashukuru Watu WA huduma ya Kwanza Nchini Redcros na Taasisi ya kupambana na majanga Nchini RAPID Kwa Kushirikiana kuadhimisha siku hiyo Mkoani Humo.

Katika hatua nyingine Chalamila ameitaka RAPID na Redcros ziendelee kujiandaa ili kuokoa maisha ya Watu yatokanayo na majanga ya maafa Nchini.


Nae Mwenyekiti WA bodi ya Rapid Maria Bilia ameiomba Serikali iweke kanuni na Sheria za kukabiliana na majanga ili maafa yasiweze kujitokeza Kwa kasi Nchini.


kwa upande Mratibu WA Redcros Kesi Ngware amesema wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu Wa Fedha na vifaa vya kutendea kazi katika kukabiliana na majanga hayo.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram