137 views 2 mins 0 comments

MJEMA:VIONGOZI WETU TUWACHUKULIE KAMA WAZAZI WETU

In KITAIFA
August 23, 2023


KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema amewataka wanachama wa chama hicho kuweza kufahamu itikadi na ilani ya chama chama cha Mapinduzi sambamba na Misingi ya chama hicho.

Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wanachama wa chama hicho jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amesema kuwa ni vyema wanachama cha Mapinduzi (CCM)wakafahamu wajibu wakuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi.


“Ukilisemea Vibaya jambo la chama chetu wenzako watalisema kwa Viongozi halafu badaye usije ukalaumu utakapochukuliwa hatua za kinidhamu,halafu ukajuta”.Alisema Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Sophia Mjema.


Mjema alisema unapotaka kulisemea jambo lazima uwe na ujuzi na hoja yakulisemea jambo hilo viongozi hawa walioshinda na wapo Katika nafasi tunataka tuwanoe


Aidha Mjema Alisema unaposema jambo lazima ujue na Maadili hajalishi ni kiongozi au mwanachama ndio uliseme jambo,tunataka kuwapa maendeleo ya chama kinataka nini,tunataka tukipeleke chama Katika mfumo wa kidigitali Zaidi Katika mfumo iliyokuwa thabiti.


“Hapa hatuna Makundi hapa tuna chama cha Mapinduzi,Nilazima uyaseme Mazuri yaliyofanywa na Mwenyekiti lazima tuwasemee viongozi wetu maana viongozi wetu wapo kama wazazi wetu”.Alisisitiza Sophia Mjema.


Mjema alibainisha kwa wanachama wa chama hicho kuwa viongozi wa chama hicho ni sawa na wazazi hupaswi kuwa semea vibaya chama Cha mapinduzi lazima kishike Tama za chama Kwa maslahi ya watanzania.


Aidha,Mjema aliongeza kuwa haipaswi kwa mwanachama wa chama hicho kuwa semea vibaya viongozi kwani viongozi wa chama hicho ni sawa na wazazi.
“Kazi yetu ni kumlinda kiongozi wetu,lazima useme Mazuri kwa mwenyekiti kuwa ametekeleza Miradi hii na uitaje” Alisisitiza Sophia Mjema

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram