Chama Cha watetezi wa haki za binadamu LHRC siku ya jumanne walizungumza kuwa dkt slaa na wezie ambao ni mwabukusi na mdude wamekamatwa Kwa kuonewa na hawakustahili kukamatwa
Sheikh mwaipopo Leo wamewajibu watetezi hao wa haki za binadamu na kusema kuwa dkt slaa na wezie hawajakamatwa Kwa sababu ya uwekezaji wa bandari
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo Alhamis 17 Agosti 2023 sheikh said mwaipopo amesema kuwa miezi 3 huko nyuma kulikuwa na sakata la uwekezaji bandari swala limekwenda na kila mmoja alikuwa na haki ya kusema na watu wengi wamesema
Mwaipopo ameshangaa kumuona mwenyekiti wa jukwaa la kikatiba la Sheria Anailea Nkya na wataalamu wengine wa kisheria kupitia kituo Cha haki za binadamu kusema kwamba Dkt.Slaa na wanasheria mwabukusi na mdude wamedhurumiwa Kwa kukamatwa Kwa sababu ya msimamo Yao ya kutetea maswala ya uwekezaji
“watu hawa hawajakamatwa Kwa sababu hiyo Bali wamekamatwa Kwa kuvunjwa amri na Sheria za nchi yetu Kuna crip slaa Alisema kuwa wataipindua serikali Kwa kumlazimisha kufanya maandamano na kusema kuwa wataiwajibisha serikali”amesema mwaipopo
“Na crip ya pili Alisema mdude kuwa watafanya na watakuja Dar es salaam Kwa kuandaa mikakati maarum ya kufanya maandamano hayo ataakikisha ataazia dodoma Dar es salaam na yatakwenda mpaka kwenye ofisi ya viongozi wa serikali ambao waliwaita ni wezie”Aliongezea mwaipopo
Alifafanua kuwa viongozi hai walitaka kwenda wakachome vituo vya polisi na wavamie ofisi za CCM na Bado wanasema kuwa hawana makosa Sheria imechukua mkono wake Kwa kukamatwa kwao na polisi ni wajibu wao Kwa kukamata watu waharifu
Na amewashangaa kituo hicho Cha haki za binadamu kuwatetea na kusema kuwa wamewaonea Kwa kukamatwa wakati wamefanya makosa
Madina Mohammed