140 views 2 mins 0 comments

ACT WAZALENDO YAIPA MBINU SERIKALI UPATIKANAJI WA MAFUTA YA PETROLI NA DISELI

In KITAIFA
August 17, 2023

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeainisha mambo matano ambayo Serikali inatakiwa kuyachukulia hatua ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta ya Petroli na Diseli nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 17, 2023 jijini Dar es Salaam Waziri Kivuli wa Sekta ya Nishati wa Chama hicho Isihaka Mchinjita amebainisha hatua hizo kuwa ni Mosi, Serikali kuweka msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya Petroli na Diseli kwa kutumia nishati mbadala ya Gesi asilia.


Kwamba hii inawezekana kwa kuchukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo magari yote ya Serikali kuanza kutumia Gesi asilia (CNG) na bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG).


โ€œVilevile, mabasi ya mwendokasi nayo yabadilishwe mfumo na yaanze kutumia gesi asilia. Pia, magari ya abiria ya mikoani (mabasi) yote yafungwe mfumo wa kutumia mitungi ya Gesi asilia (CNG), ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta,โ€ amesema Mchinjita.


Mchinjita ameeleza Pili, ni Serikali ianze kupunguza matumizi ya dola za Kimarekani kwa Benki Kuu kuruhusu wanunuzi wa mafuta kulipia kwa shilingi kisha benki hiyo ndio iwalipe wanunuzi wa nje kwa dola za Kimarekani ili kuwarahisishia wafanyabiashara ya mafuta wasihangaike kutafuta dola.
Amesema Tatu, hatua nyingine, ni kuhakikisha Serikali inadhibiti mahitaji ya dola kwa kuhakikisha matumizi yote ya ndani yanafanywa kwa shilingi ya Tanzania.

Aidha amesema changamoto ya upatikanaji wa mafuta imepeleka waagizaji wa mafuta hususani Kwa waagizaji wadogo kuchelewa kupata mzigo kutoka bohari za bandari ya Dar es salaam

“Awali iliwachukua siku Moja tu Sasa inachukua siku tatu Hadi nne kupata mafuta na kupakia Katika bohari za Dar es salaam jambo ambalo linapelekea uhaba Katika maeneo mengi”mchinjita

Hata hivyo amesema bandari ya Mtwara imekuwa mbaya Kwa mafuta ya petroli ambapo hayapatikani kabisa.jambo linalopelekea wauzaji wote waliokuwa wanachukua mafuta Katika bandari ya Mtwara kulazimika kufuata Dar es salaam

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram