Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa mwezi mmoja kwa wadaiwa sugu kulipa madeni, na kuwa watakao kaidi maelekezo hayo, watakuwa wameruhusu Shirika kuwatangaza katika vyombo vya habari ili Mashirika na makampuni mengine yasiingie kwenye makubaliano ya kibiashara na mtu au kampuni inayodaiwa.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 15, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Elias Msese, wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu deni la shilingi Bilioni 23 la shirika hilo ambalo linawadai wateja wake kwa muda mrefu.
Akizungumza kuhusu utekelezaji huo wa agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwa wateja wote wanaodaiwa kulipa fedha hizo, Meneja wa Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya, amesema Shirika limeingia mikataba na Wapangaji ya kuwaruhusu kulipa madeni hayo kwa awamu, ambapo kila mpangaji anayodaiwa atapaswa kulipa na kama ana sababu maalum ahakikishe anaweka utaratibu madhubuti wa kulipa madeni yake.
Madina Mohammed