298 views 2 mins 0 comments

CHALAMILA ASISITIZA KUTUMIA BIDHAA ZENYE KIWANGO NA SI BIDHAA FEKI

In BIASHARA, KITAIFA
August 15, 2023


ALAF Tanzania, ambayo ni moja ya makampuni chini ya Safal Group, leo imezindua rasmi dhamana ya bidhaa lengo likiwa ni kulinda ubora wa bidhaa zake kwa wateja.

Uzinduzi huu unatokana na kutapakaa kwa bidhaa zilizozalishwa chini ya kiwango na pia bidhaa bandia katika soko la Tanzania na masoko ya nje.

Meneja Masoko wa ALAF, Isamba Kasaka, alisema dhamana hiyo mpya,inalenga kuwapa walaji amani na kuwahakikishia kuhusu bidhaa za ALAF ambazo ni pamoja na mabati na nondo.

Alisema ALAF imeendelea kushtushwa na wimbi la bidhaa za chini ya kiwango na bidhaa bandia ambazo zinaathiri sekta zote nchini. “Bidhaa hizi pia ni hatari kwa usalama na afa ya walaji,” alisema.

Alisema kupitia program hii ya dhamana hii ya bidhaa wataendelea kutoa elimu kuhusu bidhaa za chini ya kiwango na feki. “Tunafanya kazi kwa karibu na serikali, vyombo vya kuimarisha sheria na vyombo vya uthibiti ili kukabiliana na wimbi hili la bidhaa feki,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Albert Chalamila, aliipongeza kampuni ya ALAF kwa kuibua mjadala huu wa bidhaa bandia. Alitoa wito kwa vyombo vyote vya usimamizi na wadau wengine wote kuimarisha vita dhidi ya wimbi hili.

Alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kama vile TBS, FCC, OSHA na nyinginezo kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora ili kuwalinda walaji.

“Walaji wanatakiwa kuichangamkia dhamana hii ya bidhaa ili wajirishishe na ubora wa bidhaa na uhalali wake kabla ya kununua,” alisema na kusiistiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu suala la ubora”Alisema mkuu wa mkoa chalamila

Kwa mujibu wa Mh. Chalamila, ukosefu wa ubora una athari kubwa za kiafya na usalama kwa walaji na wanatakiwa kulindwa.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram