122 views 19 secs 0 comments

WAKANDI NA SANLAM WASHIRIKIANA KUINUA VYAMA VYA USHIRIKA

In BIASHARA
August 14, 2023

Kampuni ya sanlam na Wakandi zimetakiwa kuendeleza kuwa Wabunifu katika kutoa bidhaa zilizobora Kwa Wananchi zitakazochagiza shughuli mbalimbali za kimaendeleo Nchini.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam mara baada ya Kamishna Mkuu WA Bima Nchini TIRA Baghayo Sakware kuzindua Bima ya Maisha ya Mkopo Wa Kigital yenye lengo la kuboresha usalama WA Fedha, ustawi WA vyama vya ushirika WA akiba na mikopo ili kuwapa fursa ya kujikinga katika hatari za Fedha kupitia Bima yenye ubora WA kipekee.


Kamishna Sakware mesema Serikali itaendelea Kushirikiana na kampuni hizo ambazo zinatumia mfumo WA kisasa unaowarahisishia huduna ziwe karibu na Wananchi.

Nae Mkurugenzi WA Kampuni ya Wakandi Francis Mwakatumbula amesema I’ma hiyo inatumia teknojia ya kisasa hivyo wameamua Kushirikiana na Sanslam katika kuzindua Bima hiyo ni kutokana na ufanisi wa kuwahudumia Wananchi Kwa muda mrefu.

Ikumbukwe kuwa Wakandi ni Kampuni inayotumia teknolojia ya kisasa katika huduma za kifedha na kuinganisha Jamii iwe karibu na fursa za kifedha kupitia teknolojia hiyo.

MADINA MOHAMMED

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram