228 views 40 secs 0 comments

FAUDHIA ACHOMWA KISU KISA KUGOMA KUOLEWA.

In KITAIFA
August 13, 2023

Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Said Mfaume (32) ambaye ni Mtaalamu wa IT na Mkazi wa Arusha kwa kumchoma na kumjeruhi Mpenzi wake aitwaye Faudhia Juma (34) Mkazi wa Singida kwa kumchoma kisu katika maeneo mbalimbali ya mwili wake kisha na yeye kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni hadi utumbo ukaning’inia akiamini kuwa Mpenzi wake amefariki kumbe bado yupo hai.

Kamanda wa Polisi Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea Aug 6, 2023 saa mbili asubuhi katika nyumba ya kulala wageni baada ya kuzuka ugomvi baina yao uliotokea baada ya Faudhia kukataa kuolewa na Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa ameshatoa mahari kwa Mama wa Faudhia huyo bila Msichana huyo kuridhia kuolewa “Baada ya Said ya kukutana na Faudhia na kujaribu kumweleza mipango ya ndoa akakataa na akatoweka Singida na kusema anakwenda kutafuta maisha”

“Said alipojua Mpenzi wake ametoroka akafanya ufuatiliaji kwa kutumia simu ya mkononi kwakuwa ni Mtaalamu wa IT na akajua Faudhia yupo Mwanza akafika Mwanza na kumuita Faudhia Gesti kisha kumchoma kisu na yeye akajichoma kisu tumboni hadi utumbo kuning’inia, pia Said tumemkuta akiwa na sumu kwenye begi”

“Kwa sasa Wapenzi hawa wawili wanaendelea na matibabu, Said anaendelea na matibabu akiwa chini ya uangalizi wa Polisi, uchunguzi ukikamilika atafikishwa Mahakamani”

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram