294 views 3 mins 0 comments

VIJANA WA JUVICUF WAIOMBA SERIKALI VIJANA WENYE MIAKA 18 KUSHIRIKI UCHAGUZI 2025

In KITAIFA
August 12, 2023

Ulimwenguni kote Leo huadhimisha kilele Cha siku ya Vijana ambayo inafanyika Katika mikoa mbalimbali Kwa Vijana Kwa kutatua matatizo Yao na kujadiliana hatima ya Vijana wa watanzania.afrika na ulimwengu mzima.

Siku hii ya Vijana Duniani ilianzishwa na umoja wa mataifa mnamo mwaka 1999 na kupitishwa Kwa Azimio namba 54/120 Kwani tarehe 12 Agosti ya kila mwaka ni maazimisho ya siku ya Vijana

Katika kuadhimisha siku ya Vijana duniani.vijana wa JUVICUF nao Leo wameazimisha siku hiyo Katika ukumbi wa Shabani Hamisi mloo uliopo Buguruni makao makuu ya CUF

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumamosi 12 Agosti 2023 katibu mtendaji JUVICUF Taifa Iddy Mkanza amesema tunafahamu juhudi zinazochukuliwa na serikali pamoja na sekta binafsi Katika kiwango Cha ukosefu wa Ajira Kwa Vijana Wenye umri wa miaka 15-24

“pamoja na muongozo huo wa kisera wizara inayohusika na maswala ya Vijana Haina mpango Wala mkakati wowote wa kupambana na changamoto zinazokwamisha juhudi za Vijana kujiajiri na kupata Ajira zenye staha”

“Mazingira magumu ya biashara yasiyo rafiki Kwa Vijana,mfano Sheria ya ushuru na Kodi TRA, BRELA ambao huleta ugumu Kwa Vijana kuanzisha na kuendesha biashara zao”.Amesema Mkanza

Mkanza amesema Katika mwaka wa fedha 2023/24 serikali itaendelea kusimamia mapinduzi ya kidijitali Nchini,tumeona serikali Bado Ina leta mzaha Kwa sababu wameshindwa kufunganisha wizara ya elimu na mafunzo na teknolojia kuwa wizara moja

Aidha uchumi wa kidijitali Afrika unatarajia kufika Dola Billioni 712 mwaka 2050 kwasasa Pato la Afrika ni Dola trilioni 3.1 ambapo uchumi wa kidijitali ni Dola Billioni 200 ambapo uwezekano mkubwa Afrika ikawa kitovu Cha uchumi wa kidijitali miaka ijayo na Tanzania ingenufaika Kwa kuongeza Ajira Kwa Vijana wake na kukuza Pato la taifa

Nae mkurugenzi wa haki za binadamu JUVICUF Raphael Ngonde amesema tukiwa tunaazimisha siku ya Vijana duniani JUVICUF tunapaza sauti Kwa serikali kuwa watanzania kutekeleza matakwa ya katiba,sheria pamoja na mikataba ya kimataifa tulioiridhia kama nchi

“kuhusu haki ya kupata taarifa na habari Ili Vijana washiriki vyema Katika maendeleo na ujenzi wa taifa lao wakiwa hawako gizani hasa hasa taarifa za mambo mbalimbali ya kitaifa kikanda na kimataifa”,

Ngonde alifafanua kuwa tunaitaka serikali kuhakikisha wanawezesha upatikanaji wa taarifa kwa Vijana ikiwemo makundi ya Vijana wenye Ulemavu kupitia lugha ya alama,utumiaji wa maandishi makubwa na maandishi ya nukta nundu serikali ifanye marejeo ya sera zinazohusu Vijana Ili kutambua mahitaji ya Vijana hasa Katika eneo la kupata ta

Hata hivyo uongozi wa Vijana wameishauri serikali ifanye marekebisho madogo ya katiba 1977 kuruhusu Vijana wenye umri wa miaka 18 kugombea ubunge na udiwani Katika uchaguzi mkuu ujao 2025 na Vijana Katika ngazi zote za maamuzi kuanzia serikali kuu na serikali ya mitaa na taasisi zingine

Madina Mohammed

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram