217 views 22 secs 0 comments

MANARA ATOA POVU KWA TIMU YA SIMBA SC

In MICHEZO
August 11, 2023

Kufuatia performance ya msanii kwenye tamasha la Simba Day iliyozua mjadala na kupelekea chama Cha watu Wenye Ulemavu ualbino kuitaka klabu ya Simba SC Tanzania kuomba radhi Kwa kitendo hicho Cha kumtumia mtu mwenye ualbino kutumika Katika tamasha hilo

Haji manara amejibu kuhusu swala hilo akiwa ni mtu anayetajwa kuhusishwa kama mlengwa wa kilichofanyika siku hiyo

Haji amesema sio mara ya kwanza kwa Simba SC kufanya kitendo kama hicho walifanya hivyo kwenye tamasha hilo la mwaka Jana na malipo ya mungu amewalipa Kwa kukosa vikombe hivyo basi kama Nia Yao ilikuwa ni kumdhalilisha yeye basi malipo yake watayapokea pia Kwa msimu huu

“Wao si wameamua kunidhalilisha na nilishangaa kweli kuona kitendo kile kilichofanywa ila me nasema kuwa kama kitendo hicho hawakunilenga mie Kwa kukusudia basi mungu mwenyewe anajua ila kama walinilenga mie basi malipo hapahapa duniani mungu atawalipia na nasema kuwa mwaka Jana walifanya hivi mungu aliwaona na hawakuchukua ubingwa ila Kwa mwaka huu tena sidhani kama watachukua ubingwa tunaona mwezi mei”.Amesema manara

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram